Story by Ephie Harusi –
Wadau katika sekta ya uvuvi mjini Kilifi wameitaka kamati inayosimamia sekta ya uchumi wa raslimali za bahari yaani Blue Economy, kuwanunulia wavuvi wa bandari ya Old Ferry vifaa vya kisasa vya uvuvi.
Mwenyekiti wa wavuvi wanaohudumu katika bandari hio Henry Chiko amesema ni lazima kamati iliyoundwa ya kufanikisha utekelezwaji wa mpango huo wa Blue Economy iwekeze katika kuwianua wavuvi hao kiuchumi.
Chiko amesema njia pekee ya kuwajenga uwezo wavuvi ni kuwapa vifaa vya kisasa vya kuendeleza shuhuli zao za uvuvi sawia na kuwatambua kama baadhi ya wafanyibiashara.
Naye Mwenyekiti wa wahudumu wa boti katika kaunti ya Kilifi Issa Shalo amesema NI lazima wavuvi wapewe mafunzo ya jinsi watakavyofanikisha shughuli zao za uvuvi.