Takribani familia 60 kutoka eneo la Malindi na ambazo zinategemea uvunjaji wa kokoto ili kujikimu kimaisha zimepokea msaada wa chakula wakati huu ambao nchi inapambana na janga la Corona.
Akizungumza baada ya ugavi wa chakula hicho,Claudia Kenga kutoka shirika la pamoja – MITANAD kutoka Austria amesema kuwa familia hizo 60 zimenufaika na unga,maharagwe,mafuta na mchele.
Claudia aidha amesema kuwa lengo lao nikuhakikisha kuwa shirika hilo linasaidia serikali katika ugavi wa chakula katika jamii mbalimbali ambazo hazina uwezo.
Mshirikishi huyo aidha amesema kuwa tayari shirika hilo limesaidia takribani familia 155 ambazo zimeathirika hata zaidi tangu janga la Corona kuripotiwa humu nchini.