Bodi ya kudhibiti filamu nchini KFCB imeapa kuwachukulia hatua kali za kisherea watengenezaji filamu ambao hawajaidhinishwa rasmi na bodi hiyo katika ukanda wa Pwani.
Afisa mkuu wa bodi hiyo ukanda wa Pwani, Boniventure Kioko, amesema kuwa imebainika wazi watengenezaji bandia hao wanaunda filamu ambazo zinakosa maadili bora ya kuelimisha jamii.
kioko aidha amewataka watengenezaji hao kujitokeza na kufuata taratibu za kupata vibali hitajika kutoka kwa bodi hiyo ili kuona kwa wanaendeleza biashara yao kwa njia sahihi.
wakati uo huo kioko amesema kama bodi tayari wameanza msako wa kuwatafuta waundaji filamu bandia huku akisema atakayepatika atakabiliwa kulingana na sheria za bodi hiyo.
Taarifa na Hussein Mdune.