Story by: Ngombo Jeff
Waumini wa Kanisa la Malindi Methodist Church kaunti ya Kilifi hatimaye wamerudi rasmi katika kanisa lao la zamani baada ya kanisa hilo kufungwa miaka mitatu iliyopita.
Kulingana na Askofu wa kanisa hilo Gambo Davies Matano, kanisa hilo lilifungwa kutokana na mzozo wa kiuongozi uliyozuka baada ya Kanisa hilo kutaka kujigatua na kuwa kanisa la Methodist la eneo la Pwani mwaka 2019.
Aidha mchungaji wa kanisa hilo Ethel Mambo amedokeza kuwa kufungwa kwa Kanisa hilo kumewalazimu waumini kushiriki ibada zao nje ya Kanisa hilo licha ya Kanisa hilo kujengwa na waumini wa eneo hilo.
Kwa upande wao baadhi ya waumini wa Kanisa hilo wakiongozwa na Katibu wao Andrew Hanjari, wameutaja mzozo wa kanisa hilo kuchangiwa na uongozi mbaya miongoni mwa viongozi wa dhehebu hilo humu nchini.