Picha kwa hisani –
Waumini wa dini ya kikristo kote nchini wamejumuika katika maeneo tofauti ya ibada usiku wa kuamkia leo ,ibada ambazo zimekamilishwa kabla ya saa nne usiku kutokana na sheria ya kafyu iliowekwa na serikali.
Hata hivyo wafuasi wa dini ya Kikristo wametakiwa kuzingatia masharti ya kiafya ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona wakati huu wa shamra shamra za Krismasi na mwaka mpya.
Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo amesema ni sharti Viongozi wa makanisa wawahimize waumini hao kuzingatia masharti hayo ili kuhakikisha waumini hao wanabaki salama.