Story by Gabriel Mwaganjoni-
Wafuasi wa dini ya Kikristu wanafanya maandamano ya amani kote nchini kuadhimisha siku ya Ijumaa njema.
Katika kaunti ya Mombasa, Askofu mkuu wa Kanisa katoliki Jimbo la Mombasa Martin Kivuva anawaongoza waumini wa Kanisa hilo katika maadhimisho hayo.
Misafara mbalimbali ya wafuasi wa Kanisa Katoliki imeshuhudiwa katika maeneo tofauti kaunti ya Mombasa huku wakibeba msalaba kuashiria kumbukumbu ya mateso aliyopitia Yesu Kristu mwana wa Mungu kulingana na Imani ya dini hiyo.
Baadaye, Wakstiru walirudi makanisa mwendo wa adhuhuri na kuendelea na ibada ya kumbukumbu taratibu za mateso aliyopitia yesu Kristu zinazotajwa kama msingi wa Imani wa dini hiyo.
Ijumaa njema inatangulia ibada ya mkesha wa Pasaka siku ya Jumamosi, na kuendelea kwa sikukuu ya Pasaka hadi Jumatatu ili kuashiria ufufuko wa Yesu Kristu ambao ndio msingi wa imani wa dini ya Kikirstu kote ulimwenguni.