Picha kwa hisani –
Viongozi wa vyama vyote vya madaktari nchini wamefanya kikao cha faragha na madaktari katika kaunti ya Mombasa,kujadiliana kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea katika kaunti hio sawa na changamoto za madaktari wote nchini.
Akizungumza baada ya kikao hicho katibu mkuu wa chama cha madaktari nchini KMPDU Dkt Mwachonda Chibanzi amesema madaktari wote hadi wale wa vituo vya kibnafsi watajiunga kwenye mgomo iwapo serikali za kaunti zitaendelea kuwapuuza.
Dkt Chibanzi vile vile ameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kutekeleza matakwa ya madaktari wa kaunti hio,akisema hatua ya serikali ya kuwaachisha kazi madaktari wanaogoma ni kinyume cha sheria.
Siku ya jumatano juma hili serikali ya kuanti ya Mombasa iliwaachisha kazi madaktari 86 katika kaunti hio baada ya kushiriki mgomo kuanzia tarehe 2 mwezi disemba mwaka uliopita.