Picha kwa hisani –
Wauguzi katika kaunti ya Mombasa wanaishinikiza Serikali kuliwajibikia swala la malipo yao.
Wauguzi hao wamesema Serikali ya kaunti hiyo imewahangaisha na kushindwa kuwalipa mishahara na marupurupu yao kwa wakati ufaao hali inayowafanya wauguzi hao kuishi katika maisha ya taabu.
Katibu wa Muungano wa wauguzi katika kaunti hiyo Peter Maroko amesema mgogoro huo wa malipo umelemaza sekta ya afya katika kaunti ya Mombasa.
Maroko amesema licha ya wauguzi hao kujadiliana na wahusika katika Serikali ya kaunti hiyo, lalama zao kuhusu malipo zimepuuzwa.