Watu walio na akili tahira katika Kaunti ya Mombasa wako katika tishio kubwa kwenye suala la maambukizi ya virusi vya Corona miongoni mwa wakaazi wa Kaunti hiyo.
Mwenyekiti wa kundi la akina Mama la ‘Women Empowerment Network’ Bi Amina Abdallah amesema ni sharti watu hao wasiachwe nje katika mikakati ya kulikabili janga hilo.
Kulingana na Bi Abdallah, watu hao vile vile wanahitaji tiba na usaidizi maalum akihoji kwamba wanapitia hali ngumu hasa ukosefu wa chakula.
Bi Abdallah amesema kundi hilo la akina Mama linajizatiti ili kuwakimu wale watakaorudi hali yao ya kawaida baada ya matibabu na ushauri ili wajiunge tena na familia zao.