Story by Mercy Tumaini –
Watu wawili wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Rabai kaunti ya Kilifi baada ya kupatikana wakijihusisha na biashara ya pombe haramu ya Chang’aa.
Kamanda wa polisi eneo la Rabai Fred Abuga amesema katika oparesheni ya kusaka pombe haramu wamefanikiwa kunasa lita 220 za pombe ya Chang’aa na kumwanga Kangara lita 480 huku washukiwa wengine wakifanikiwa kutoroka.
Abuga amesema oparesheni hiyo litaendelea ndani ya Rabai ili kuhakikisha wale wanaofanya biashara ya vileo wanazingatia sheria na kuuza pombe iliyoidhinishwa.
Kwa upande wake Msaidizi wa Naibu Kamishna wa Rabai Maryane Nduati amewasihi Akina mama wanaojihusisha na biashara ya Chang’aa kusitisha biashara hiyo na kuanzisha biashara zengine za kujipatia riziki kila siku.