Watu watatu wamenusurika kifo baada ya gari lao kuteketea katika ufukwe wa Bahari hindi wa Shelly huko Likoni Kaunti ya Mombasa.
Walioshuhudia tukio hilo lilitokea karibu na hoteli ya ‘Kwetu Beach resort’ wamesema watatu hao waliokua ndani ya gari dogo aina ya V8 wamepeleka gari hilo kwenye ufuo huo wa Bahari kabla ya kukwama kwenye matope.
Kulingana na maafisa wa usalama watatu hao walikuwa wameenda kujivinjari na kuliwasha gari hilo huku wakilisukuma ili kulikwamua kuwenye tope ufukweni,hali iliyopelekea injini ya gari hilo kuwaka moto na kuteketeza gari hilo na kulisaza jivu.
Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo la asubui ya leo.