Watu watatu wameaga dunia mmoja akiachwa na majeraha mabaya baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani katika barabara ya Kombani – Kwale asubui ya leo.
Kamishna kaunti ya Kwale Joseph Kanyiri amesema ajali hio imetokea baada ya dereva wa lori iliyokua na shehena ya mitungi ya gesi alipojaribu kuipita tuktuk iliokua inaelekea upande sawa na lori hio,kabla ya kuingonga tuktuk nyengine iliokua inaelekea upande tofauti.
Kanyiri ameeleza kwamba dereva wa lori hio anazuiliwa na maafisa polisi uchunguzi ukiidhinishwa kubaini chanzo cha ajali hio,akiwasihi madereva kuwa makini kwani barabara hio ina utelezi kutokana na mvua inayoshuhudiwa.
Miili ya watatu hao inahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya mjini Kwale,huku aliyejeruhiwa akiendelea kupokea matibabu ya dharura katika hospitali hio.