Shughuli za kawaida zimetatizwa katika barabara ya Mombasa -Voi-Nairobi baada ya gari moshi la kubeba mizigo kugongana na basi la kubeba mizigo la kampuni ya WellsFargo katikati mwa mji wa Voi.
Kamanda wa polisi wa eneo la Voi Patrick Okeri amesema dereva wa basi hilo hakupeyana nafasi ya gari moshi kupita hali iliosababisha ajali hiyo na kuwajeruhi watu wanne.
Okeri amemlaumu dereva wa basi la kampuni ya WellsFargo kwa kutokuwa makini barabarani na kusababisha ajali hiyo, akifahamu wazi kwamba gari moshi lilimuashiria kutaka kupita.
Japo hakuna maafa yoyote yalioripotiwa katika ajali hiyo, watu wanne waliojiruhiwa wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi.
Wakati uo huo madererva wa magari ya uchukuzi wa umma, kibinafsi na masafa marefu wamehimizwa kuwa makaini zaidi babarani ili kuepuka ajali.