Watu wanane wamejeruhiwa vibaya jioni ya leo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani kwenye barabara kuu ya kutoka Malindi kuelekea Lamu.
Basi hilo la Kampuni ya Tawakal lilipinduka katika eneo la Witu kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo.
Kamanda mkuu wa polisi kaunti ya Lamu Muchangi Kioi amesema Dereva wa basi hilo lililotoka Mombasa asubuhi ya leo likielekea Lamu alishindwa kulidhibiti kutokana na utelezi katika barabara hiyo.
Hata hivyo Muchangi amesema abiria wengine wamepata majeraha madogo na wakaruhusiwa kuchukua basi lingine ili kuwasafirisha hadi eneo la Mokowe huko Lamu.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.