Watu wanne wamefariki na wengine wanane kujeruhiwa baada ya matatu waliyokuwa wakisafiria kugonga lori la kampuni moja ya saruji katika eneo la Shaurimoyo barabara kuu ya Mombasa – Malindi.
Wanne hao ni pamoja na dereva wa matatu hiyo na abiria wengine wa kike.
Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo , lori hilo limesimama ghafla na kupelekea matatu hiyo kuigonga kutoka kwa nyuma.
Afisa mkuu wa polisi mjini Kilifi Njoroge Ngigi amethibitisha ajali hiyo huku miili ya abiria waliofariki ikihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu ya Kilifi.
Taarifa na Marieta Anzazi.