Picha kwa hisani –
Watu wanane wameaga dunia wengine wawili wakiachwa na majeraha mabaya baada ya matatu walilokua wakisafiria kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Soysambu huko Gilgil kwenye barabara kuu ya Nairobi -Nakuru.
Kamanda mkuu wa polisi eneo la Gilgil John Onditi amesema matatu hio iliokua ikitoka Nakuru kuelekea Nairobi ilikuwa na abiria kumi kabla ya kugongana ana kwa ana na trela na kwamba ni abiria wawili pekee walionusuruka
Odinti aidha amesema manusura hao wawili wa ajali hio iliyotokea asubui ya leo tayari wamekimbizwa katika hospitali ya St Mary’s kwa ajili ya matibabu ya dharura.
Onditi amesema hakuna msongamano wa magari unaoshuhudiwa katika bara bara hio ya Nairobi – Nakuru kwani maafisa wa trafiki wamefanikiwa kuyaelekeza magari yanayotumia barabara hio.