Kamishna kaunti ya Kilifi Magu Mutindika amewataka wakaazi wa kaunti hio kushiriki zoezi linaloendelezwa la usajili watu la huduma namba.
Akizungumza na wanahabari mjini Kilifi Mutindika amesema wanatarajia kusajili watu milioni 1.4 katika kaunti ya kilifi kwenye mpango huo na kufikia sasa wamesajili watu elfu 87,694 .
Kwa upande wake kaimu chifu wa ngerenya Tecla chai amesema kuwa kuwa hitilafu za vifaa na dhana potovu ni miongoni mwa changamoto zinazokumba zoezi hilo.
Lucy Chiru mmoja wa waliosajiliwa katika mpango huo katika kituo cha Ngerenya amepongeza zoezi hilo.