Huenda zaidi ya watu 700 wakapoteza ajira iwapo kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium itasitisha shughuli zake ifikapo mwaka wa 2022.
Afisa msimamizi wa miradi ya jamii katika kampuni hiyo Juma Lumumba ameeleza wasiwasi kuwa iwapo kampuni hiyo haitapata sehemu mbadala ya kupanua shughuli za uchimbaji madini, wakaazi wengi watapoteza ajira na ufadhili wa karo kwa wanafunzi.
Wakati uo huo Lumumba amepuuzilia mbali madai kuwa zoezi la uchimbaji madini limewaathiri wakaazi kiafya, akitaja madai hayo kama dhana zisizothibitika.
Amekariri kuwa hakuna wafanyikazi wa kampuni hiyo ambao wamelalamika kuathirika tangu uzinduzi wa uchimbaji madini eneo hilo.
Taarifa na Michael Otieno.