Jopo la watu 7 walioteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kuwapiga msasa wakenya waliotuma maombi ya kujaza nafasi za Makamishna wanne wa Tume ya huru ya uchaguzi na mipakani nchini IEBC wamekula kiapo.
Watu hao 7 ni pamoja na Gideon Solonka, Dkt Elizabeth Muli, Awori James Achoka, Elizabeth Odundo Meyo, Kasisi Joseph Ngumbi na Dkt Faradim Suleiman Abdullah.
Hata hivyo Dorothy Kimengech ambaye ni mtu wa 7 katika jopo hilo amekosa kufika katika majengo ya Mahakama ya Upeo kula kiapa na idadi hiyo kusalia watu 6 ambao wanatarajiwa kuanza vikao vya kuwapiga msasa watu wanaotaka kujaza nafasi za makamishna wanne wa IEBC waliojiuzulu.
Akizungumza baada ya kushuhudia jopo hilo likila kiapo, Naibu Jaji mkuu nchini Philomena Mwilu amewashauri watu hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa uwazi na kuwateua makamishna watakaosimamia uchaguzi mkuu kwa njia ya haki.