Picha kwa hisani –
Kamati inayoshughulikia ugonjwa wa corona katika kaunti ya Kwale imethibitisha kwamba kufikia sasa watu watatu wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa corona katika kaunti hio.
Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa kamati hio Gavana Salim Mvurya amesema wagonjwa wawili wa corona wanaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya Msambweni na wengine sita wakiwa tayari wamepona virusi hivyo.
Gavana huyo wa Kwale ameeleza kwamba kufikia sasa hakuna shule iliyoripoti maambukizi ya virusi vya corona katika kaunti hio akiwasihi wazazi kuchukua jukumu la kuwalinda watoto wao na maambukizi.
Kwa upande wake kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Joseph Nthenge amewasihi wakaazi wa kaunti hio hasa wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma kuzingatia maagizo ya kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.