Picha kwa hisani –
Watu 263 wamethibitishwa kupata maambukizi ya virusi vya corona baada ya sampuli za vipimo 4,424 kufanyiwa uchungizi ndani ya saa 24 na idadi hiyo kuongezeka hadi watu 34 057.
Kwenye taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe, taarifa hiyo imesema kuwa kati ya watu hao 263, watu 259 ni wakenya na wengine wakiwa raia ya kigeni.
Taarifa hiyo imesema kuwa watu 180 ni wanaume huku 83 wakiwa wanawake na mtoto wa umri wa mwaka mmoja ni kati ya walioambukizwa virusi vya Corona,.
Hata hivyo watu 98 waliokuwa wakiugua virusi vya Corona wamethibitishwa kupona na kupelekea idad hiyi kufikia watu 19,688 huku watu wawili wakiaga dunia.