Picha kwa hisani –
Jumla ya watu 22 wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya watu wawili katika eneo la Madogo Kaunti ya Tana river wametiwa nguvuni.
Kulingana na Mshirikishi mkuu wa utawala Kanda ya Pwani John Elungata oparesheni hiyo itaendelea hadi jamii mbili za Wamunyoyaya na Waorma zinazochangia uhasama huo zikumbatie amani.
Elungata aidha, amezipa jamii hizo muda wa siku mbili pekee kurudisha mifugo waliyoibwa wakiwemo mbuzi 48.
Elungata aliyeongoza vikao vya usalama na amani kwa siku nzima hapo jana katika eneo la Madogo lililoko kwenye mpaka wa Kaunti za Tana River na Garissa amesema vikosi vya usalama vitakita kambi katika eneo hilo hadi pale hali itakapokuwa shwari.