Picha kwa hisani –
Wizara ya afya nchini imethibitisha kwamba watu 21 wameaga dunia ndani ya saa 24 zilizopita kutokana na virusi vya corona nchini na sasa idadi kamili ya vifo vinavyotokana na corona imefikia elfu 1 na 93.
Katika taaarifa kwa vyombo vya habari waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe vile vile amethibitisha kwamba watu elfu 1 ,109 wamepata maambukizi ya virusi vya corona hii leo baada ya sampuli elfu 7,153 kukaguliwa.
Kagwe amesema wagonjwa elfu 1, na 73 kati yao ni raia wakenya huku wagonjwa 36 wakiwa raia wa kigeni na kwamba kufikia sasa kenya ina jumla ya visa elfu 60,704 vya maambukizi ya corona.
Kagwe vile vile amethibitisha kwamba wagonjwa 938 wa corona wamepona virusi hivyo na kwamba wagonjwa 856 kati yao walikua wanahudumiwa nyumbani na sasa waliopona corona nchini imefikia watu elfu 40,131.