Story by Janet Shume-
Watu 16 wanauguza majeraha katika hospitali ya Mariakani baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani kwenye barabara kuu ya Nairobi -Mombasa katika eneo la Samburu kaunti ya Kwale.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo,Afisa mkuu wa polisi eneo la Samburu Fredrick Ombaka amesema ajali hiyo imehusisha magari matatu ikiwemo gari la abiria ya kampuni ya Naekana na malori mawili.
Ombaka amesema ajali hiyo imetokea baada gari hilo la abiria lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea Mombasa kujaribu kukwepa gari bovu lililokuwa limeegeshwa barabarani baada ya gari lengine kukosa mwelekeo na kuligonga gari hilo la abiria na kusababisha ajali hiyo.