Watu 13 wamejeruhiwa vibaya baada ya kushuhudiwa kwa mkanyagano katika kivuko cha feri cha Likoni kule kaunti ya Mombasa mapema leo jioni.
Mkurugenzi wa Shirika la hudumu za feri nchini Bakari Hamis Gowa amesema mkanyagano huo umetokea baada ya feri ya Mv Kwale kuigonga feri ya Mv Safari na kutoboa shimo katika feri hiyo hali iliopelekea maji kuingi katika ingini ya feri hiyo.
Gowa amesema juhudi za wahudumu wa kivuko cha feri cha Likoni wamefanikiwa kuikwamua feri hiyo huku baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wakisema kilichosababisha mkanyagano huo ni kucheleweshwa kwa watu kuingia kwa feri wakihofia usalama wao.
Hata hivyo maafisa wa Shirika la Msalaba mwenduku kaunti ya Kwale waliwasili katika kivuko hicho na kuwasaidia watu walijeruhiwa kufuatia tukio hilo.