Picha kwa hisani –
Watu 10 wanahofiwa kuaga dunia baada ya boti walilokuwa wakisafiria kupenduka huko Usenge katika ziwa Victoria usiku wa leo.
Kulingana na mwenyekiti wa usimamizi fuo za ziwa eneo hilo, Eli Odhiambo Masinde, Boti hilo la mizigo ilikua inatoka eneo la Nairobi Uganda na kuelekea Usenge na lilikuwa na takriban abiria 20.
Kufikia sasa bado shughuli za kuokoa manusura zinaendelea huku tayari watu kumi wakiwa wameokolewa akiwemo mtoto wa miaka mitatu.
Kulingana na manusura, ajali hiyo imesababishwa na upepo mkali kufuatia mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.