Picha kwa Hisani –
Watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka mitatu na mitano wameaga dunia baada ya kuteketea kiasi cha kutotambulika katika eneo la Maluwani huko Kaloleni kaunti ya Kilifi.
Afisa mkuu wa polisi eneo hilo Ezekiel Chepkwony amethibisha mkasa huo akisema moto huo umezuka mwendo wa saa kumi na mbili alfajiri ya leo baada ya watoto hao kuachwa na mama yao aliekua akikimbilia hospitali kumpeleka mtoto wake mwengine.
Kwa upande wake mzee wa mtaa wa kwa kidunga ajeni Charles Karisa amesema kuwa amepata taarifa hizo kutoka kwa majirani na alipofika eneo la mkasa tayari moto umesambaa katika chumba walimokua wamelala watoto hao.
Tayari maafisa wa polisi wameidhinisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo huku miili ya wawili hao ikihifadhiwa katika hospitali kuu ya Kilifi.