Afisa wa kitengo cha upelelezi wa jinai anayekabiliana na ulanguzi wa mihadarati katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi mjini Mombasa Josiah Nyabere amethibitisha kuwepo kwa walaghai wanaoweka dawa za kulevya kwa vinywaji kwa lengo la kuwalaghai wananchi.
Nyabere amesema kuwa watu hao wanaweka dawa za kulevya kwa vinywaji na chakula kabla ya kuendeleza vitendo vya kihalifu kwa wahusika.
Nyabere ameitaka jamii na hasa watoto kutokubali vyakula na vinywaji kutoka kwa watu wasiowafahamu.
Nyabere amesema kuwa wakati huu wa likizo watoto wako katika hatari ya kuhusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya akisema mara nyingi wanafunzi wamekuwa wakitumiwa kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya.
Taarifa na Mariam Gao.