Picha kwa hisani –
Shirika linaloangazia masuala ya wanawake la Kilifi Mums limesema watoto wa kiume wanaolawitiwa hawana ujasiri wa kujitokeza kuripoti visa hivyo kama ilivyo kwa wenzao wa kike.
Akizungumza na mwanahabari wetu mwenyekiti wa shirika hilo Bi Kibibi Ali ametaja hofu ya kejeli kutoka kwa jamii kama baadhi ya mambo yanayozuia watoto wa kiume kuripoti visa hivyo.
Bi Ali aidha amesema watoto wa kiume wanaodhulumiwa hupokea vitisho kutoka kwa wale wanaowatendea unyama huo.