Shirika la Afya duniani WHO limesema kuwa takribani watoto million 250 kote duniani chini ya miaka 8 wapo katika hatari ya kukumbwa na maradhi yanayoambatana na ukosefu wa lishe bora.
Akihutubu kongamano la kitaifa la wadau kuhusu maendeleo ya watoto, afisa wa maendeleo ya watoto kutoka shirika la afya duniani WHO Martini Chabi, amesema kuna haja ya wazazi kuzingatia kwa umakini afya ya watoto kutoka wanapozaliwa ili kuhakikisha wanakuwa katika hali iliyo bora kiakili na kiafya akitaja ukosefu wa lishe bora kwa watoto huchangia ukuaji hafifu wa kiakili jambo linalowapelekea kukosa uwezo wa kufanya vyema hata masomoni mwao.
Amesema ili kufikia malengo ya elimu bora, afya bora pamoja na kupunguza umasikini ukuaji wa mtoto ndio eneo ambalo linastahili kutiliwa mkazo zaidi.
Wakati uo huo mwenyekiti wa mtandao wa elimu ya chekechea (ECD) Teresa Mwona amesema ili kulinda hali ya baadaye ya watoto nchini ni jukumu la serikali pamoja na wadau mbali mbali kushiriana ili kuhakikisha kuna utaratibu wa kisheria kahusu maendeleo ya watoto.