Watetezi wa haki za kibinadamu katika kaunti ya Tana river wameikosoa Serikali ya kaunti hiyo kwa kuitelekeza sekta ya afya.
Wakiongozwa na Afisa wa nyanjani wa Shirika la MUHURI Ogle Abdi, Watetezi hao wamesema wagonjwa katika hospitali ya Ngao kaunti ya Tana river wamekuwa wakihangaika kwa kukosa huduma za matibabu hospitalini humo.
Kulingana na Abdi, licha ya hali hiyo kukithiri kwa zaidi ya miezi sita sasa, hakuna hatua zozote zilizoekezwa na Serikali ya kaunti hiyo katika kuiboresha sekta ya afya
Mtetezi huyo wa haki za kibinadamu amesema atajumuika na Watetezi wengine na kufanya maandamano ili kuishinikiza Serikali ya kaunti hiyo kuwajibikia majukumu yake ya kuboresha sekta ya afya.