Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.
Mombasa, Kenya Mei 23 – Kamanda mkuu wa Polisi Kaunti ya Mombasa Johnston Ipara amewataka polisi kuwatia nguvuni mara moja watetezi wa haki za binadamu wanaoneza habari za uongo kuhusiana na swala la usalama katika Kaunti hiyo.
Ipara amesema kwamba wanaharakati hao wamekuwa wakiendeleza habari za uchochezi kwamba wakaazi wa eneo la likoni wanadungwa sindano na wahalifu kama mbinu mpya ya kutekeleza uhalifu katika eneo hilo.
Akizungumza katika eneo la Shika adabu huko Likoni, Ipara amesema kwamba baadhi ya mashirika hayajatekeleza majukumu yao kikamilifu katika kushirikiana na idara ya usalama na wakaazi wa kaunti hiyo kuhakikisha maswala msingi ya kijamii yanatiliwa mkazo.
Kwa upande wake Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki ameyakosoa baadhi ya mashirika ya utetezi wa haki za kibinadamu kwa kutowajibika majukumu yao.