Story by Gabriel Mwaganjoni
Kinara wa Chama cha Ford-Kenya Moses Wetangula amemtaka Waziri wa fedha nchini Ukur Yattan kukoma kuwahadaa wakenya kwamba uchumi wa nchi umeimarika kwa asilimia 7.5.
Wetangula amesema huo ni uongo mtupu na Serikali inapaswa kuwaambia wakenya ukweli kwamba taifa hili linapitia msukosuko mkubwa wa kiuchumi unaostahili kurekebishwa.
Akizungumza katika eneo la Magharibi mwa Kenya wakati wa mikutano ya kisiasa ya Kenya Kwanza Wetangula amewataka wakenya kuegemea mrengo wa Kenya Kwanza ili kufanikisha mabadiliko ya uhakika ya kiuchumi.
Kauli yake imeungwa mkono Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi aliyehoji kwamba wakenya hawatajutia pindi watakaposhirikiana na mrengo wa Kenya Kwanza na kumchagua Naibu Rais Dkt William Ruto kama rais wa taifa hili ifikapo Agosti, 9.