Serikali ya kaunti ya Mombasa imehimizwa kuwakabili vikali watu wenye tabia ya kuwatumia walemavu kama kitega uchumi barabarani.
Kulingana na Mwakilishi wa Kike kaunti ya Mombasa Asha Hussein, idadi ya watu wanaozurura na walemavu barabrani imezidi kuongezeka katikati ya miji mikuu katika kaunti hiyo huku akitaka swala hilo likomeshwe mora moja.
Amesema ni bora zaidi endapo walemavu watafunguliwa biashara ndogo ndogo ili wajikimu kimaisha bala ya kutumiwa vibaya na baadhi ya watu fulani kujipatia mapato.
Taarifa na Hussein Mdune.