Taarifa na Dominick Mwambui
Kwale, Kenya, Julai 4 – Watangazaji wa Radio Kaya wameitunuku shule ya wanafunzi wa mahitaji maalum kutoka Kwale.
Watangazaji hao wakiongozwa na Mrinzi Nyundo wameitunuku shule hiyo vifaa vya kutumia katika mashindano ya mziki mwaka huu.
Shule hiyo ilifuzu kwa hatua ya kitaifa ya mashindano ya mziki baada ya kuimbuka ya pili ukanda wa Pwani. Mwezi Agosti itahitajika kusafiri hadi katika shule ya upili ya Kabarak ambako watawakilisha ukanda wa Pwani.
Akizungumza wakati wa ziara yao shuleni humo, Mrinzi amesema kuwa waliitunuku shule hiyo kutokana na juhudi zake za kudumisha utamaduni wa kimijikenda.
“Densi zenu mbili za Gonda na Chechemeko zimeuvutia sana na tumeona ni vyema tuwe na mchango katika safari yenu ya kuzidi kudumisha utamaduni wa kimijikenda,” amesema mtangazaji huyo.
Kwa upande wake mwalimu anayehusika na somo la mziki katika shule hiyo, Anastacia Kanga amesema kuwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wana uwezo mkubwa lakini jamii imewatenga kiasi cha kwamba wanaishi kwa kuteseka.
“Hawa watoto wapo ma uwezo mkubwa sana. Iwapo jamii itawaunga mkono basi wanaweza kufanya mambo makuu. Kwa sasa tunaomba wahisani wema wajitokeze ili watusaidie katika safai ya haya mashindano ya kitaifa. Tuna imani tutashinda,” amesema mwalimu huyo.
Kwa sasa shule hiyo inahitaji mavazi rasmi ya kimijikenda ili kuyatumia katika mashindano hayo.