Mazingira duni baharini na katika fuo za bahari Mombasa unahofiwa kuwasababisha watalii wengi kutozuru kaunti ya Mombasa.
Kwa mujibu wa Janet Morobi mshikadau katika sekta ya utalii Pwani, ni vyema kwa serikali ya kaunti ya Mombasa kulipa kipaumbele swala la usafi wa bahari ili kuimarisha viwango vya utalii.
Aidha ameitolea mwito mamlaka ya bandari nchini KPA kuzingatia usafi wa baharini ili kuimarisha kiwango cha watalii wanaozuru Pwani akisema watalii wengi kwa sasa wanazuru zaidi Pwani kusini kutokana na uwepo wa bahari na fuo safi eneo hilo.
Amehimiza kuidhinishwa kwa mpango wa kutumia vijana kusafisha bahari na mazingira ya bahari ili kuweka mazingira bora kwa watalii.
Taarifa na Hussein Mdune.