Story by Ephie Harusi-
Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya kuajiri walimu nchini TSC Nancy Macharia amewasihi watahiniwa wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE kutohofia lolote na badala yake kuzingatia waliyofunzwa na walimu.
Akizungumza katika kaunti ya Kilifi baada ya kushuhudia ufunguzi wa makasha ya mtihani huo, Nancy amewarai wanafunzi hao kutokubali kushawishiwa vibaya na kushiriki udanganyifu wa mitihani.
Nancy amewataka walimu na wasimamizi wa mitihani hiyo kuhakikisha wanawajibikia majukumu yao vyema ili kuzuia kushuhudiwa kwa wizi wa mitihani, akisema ni lazima zoezi hilo liendeshwe vyema.
Kwa upande wake Kamishna wa kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka ameunga mkono kauli hiyo, akiwataka wasimamizi wa mitihani hiyo kuwa waangalifu zaidi sawa na kuzingatia sheria za mitihani.
Kauli za viongozi hao zimejiri siku chache tu baada ya mwanafunzi mmoja katika shule ya upili ya Takaungu kaunti ya Kilifi kupatikana na simu ya rununu wakati wa mitihani hiyo.