Maafisa wa kupambana na ufisadi tawi la Malindi wamefaulu kuwakamata washukiwa watatu wanaodaiwa kuhusika kwa wizi wa vitabu vya serikali.
Akithitbitisha kukamatwa kwa watatu hao ambao kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Malindi afisa mkuu wa tume hiyo kanda ya Pwani Gichangi Njeru amesema kuwa mmoja wa washukiwa hao aliyetambuliwa kwa jina Philip Kimaro anayesimamia shule ya kibinafsi ya Marys Junior eneo la Soweto mjini Malindi amepatikana akiwa na dazani nyingi za vitabu vya serikali.
Njeru aidha amehoji kuwa vitabu hivyo vya aina mbali mbali vya shule ya msingi vinadaiwa kuibwa kutoka kwa shule za serikali na hata kubadilishwa mihuri na kuwekwa mihuri ya shule hiyo ya kibinafsi.
Afisa huyo amesema kuwa washukiwa wawili waliokamatwa ni walimu wa shule za msingi ambao wanadaiwa kuiba vitabu hivyo ambavyo ni mali ya umma na kuviuza kwa msimamizi wa shule hiyo ya kibinafsi.
Taarifa na Charo Banda.