Chama cha Wamiliki wa matatu Kanda ya Pwani kitaongeza nauli kuanzia tarehe mosi ya Mwezi Septemba mwaka huu.
Hii inafuatia hatua ya Serikali kuweka asilimia 16 ya ushuru unaotozwa mafuta yanayoingizwa humu nchini. Ushuru utakaoanza kutozwa rasmi terehe mosi Mwezi Septemba mwaka huu.
Akitoa tangazo hilo Mjini Mombasa hii leo, Mshirikishi mkuu wa Chama hicho Kanda ya Pwani Salim Mbarack Salim amesema kwamba nauli za Kaunti ya Mombasa zitaongezeka kwa shilingi 10 katika kila barabara huku zile za nje ya Mombasa kutoka Kaunti moja hadi nyingine zikiongezeka kwa shilingi 50.
Serikali kupitia kwa tume ya kudhibiti kawi nchini (ERC) iliondoa ushuru wa mafuta yanayoingizwa humu nchini kwa kipindi cha miaka mitano, kipindi hicho kinakamilika tarehe 31 ya mwezi Agosti mwaka huu.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.