Taarifa na Gabriel Mwaganjoni
Mombasa, Kenya Oktoba 22 – Vijana 50 waliojinasua kutoka kwa uraibu wa mihadarati watafaidika na mradi wa “Skills mtaani”, amesema Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir.
Mradi huo unalenga kuwakimu vijana kwa namna mbalimbali za kupata ujuzi na kujitegemea.
Nassir amesema vijana watanufaika na ufadhili wa masomo katika awamu yake ya nne itakayozinduliwa Disemba mwaka huu ili wajipatie ujuzi na kuidhinisha miradi yao ya kimapato.
Nassir ameitaja hatua hiyo kama itakayowaondoa waraibu hao katika hali hiyo ya kusikitisha, akisema Mabinti waliyojinasua kutoka wa uraibu huo watapewa kipau mbele ili kuwazuia kuregelea tena uraibu huo.
Akiwahutubu katika mkao wa hamasa kuhusu athari z utumzii wadawa kulevya katika eneo bunge lake, Nassir amewataka Maafisa hao wa nyanjani kuwabadili waraibu na kuwafanya kuwa Mabalozi wa kulikabili janga hilo katika jamii.