Story by Ali Chete-
Jamii ya ukanda wa Pwani imehimizwa kuacha mila na desturi zilizopitwa na wakati na kuwapa nafasi wanawake katika nyadhfa za uongozi.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Sports Connect Athanus Mdoe Tangai amesema wakati umefika sasa kwa wakaazi kutambua juhudi zinazoendelezwa na wanawake mashinani na kuwapa nafasi ya kunyakua viti vya kisiasa.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Tangai amesema juhudi zilizopigwa na wanawake katika sekta mbalimbali nchini zimeonysha wazi kwamba wanawake wana uwezo wa kushikilia nyadhfa mbalimbali za uongozi nchini na kuchangia maendeleo.
Wakati uo huo amewahimiza Wanawake kujitokeza na kupigania nyadhfa za uongozi ili kuwasaidia wananchi katika kunufaika na miradi ya maendeleo.