Afisa mkuu wa bodi ya filamu nchini kanda ya Pwani Boniventure Kioko amewatahadharisha wakaazi wa maeneo ya mashinani wanaoendeleza biashara ya michezo ya kamari kwamba watakabiliwa.
Akiongea mjini Mombasa Kioko amesema kuwa wamiliki wengi wa mashini za mchezo wa kamari wamezihamisha sehemu za mashinani kuendeleza biashara hio na kuwapotosha watoto wenye umri mdogo.
Kioko amesema kuwa wanapanga kufanya msako mkali wa kusaka na kusambaratisha mashini hizo akisema kuwa zimewafanya watoto wengi kuwa wezi na kutozingatia masomo yao.
Hata hivyo amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao hususan kipindi hiki cha likizo ya mwisho wa mwaka ilikuona kwamba hawajihusishi na mambo yasiofaa.
Taarifa na Hussein Mdune.