Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Safina Jimi Wanjigi amekemea mauaji ya kiholela na kupotezwa kwa watu humu nchini akiitaja hali hiyo kama ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Akizungumza jijini Nairobi Wanjigi amesema ni sharti taifa hili lipate mwelekeo tofauti kuhusu mauaji ya kiholela na utumizi wa nguvu kupita kiasi dhidi ya wakenya.
Wanjigi amewataka viongozi wa kidini kushirikiana na viongozi walio na nia ya kulitanzua swala hilo ili unyama huo ambao umekithiri humu nchini ukomeshwe.
Wakati uo huo amesisitiza kwamba Serikali ina ufahamu wa kina kuhusu polisi wanaowateka na kuwapoteza wakenya hasa katika maeneo ya Nairobi, Kaskazini Mashariki mwa nchi na Pwani.