Story by Our Correspondents
Mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Safina Jimi Wanjigi, amejitokeza na kuikosoa serikali ya Jubilee kwa madai kwamba imeshindwa kukabiliana na swala tata la ufisadi nchini.
Akizungumza na Wanabahari baada ya kufanya mikutano kadhaa ya kisiasa katika kaunti ya Kiambu, Wanjigi amesema viongozi wa Muungano wa Azimio na Kenya kwanza hawana ajenda za kupambana na ufisadi nchini.
Wanjingi amewataka wakenya kuwa waangalifu dhidi ya viongozi hao, akisema hawana mipango ya kukomesha ufisadi nchini kwani viongozi hao ni kati ya wale wanaohusika na kashfa za ufisadi.
Wakati uo huo amewataka wakenya kuunga mkono azma yake ya kuwania kiti cha urais humu nchini akisema ameweka mikakati mwafaka ya kuhakikisha taifa hili linapiga hatua kiuchumi na maendeleo sawa na kukomesha ufisadi nchini.