Taarifa na: Ephie Harusi
Kilifi, Kenya, Juni 11 – Wanawake wawili wanazuiliwa katika kituo cha polisi mjini Kilifi baada ya kupatikana na zaidi ya misokoto elfu 2600 ya bangi katika operesheni inayoendelezwa dhidi ya walanguzi wa mihadarati katika kaunti hiyo.
Akithibitisha kukamatwa kwao afisa mkuu wa polisi Kilifi kaskazini Patrick Njoroge amesema polisi wamepashwa habari na wananchi na kufanikiwa kuwanasa washukiwa na bangi hiyo yenye thamani ya shilingi 300,000.
Njoroge amesema polisi wataendelea na oparesheni ya kuwasaka walanguzi wa mihadarati kuhakikisha biashara hio inasambaratishwa kaunti nzima ya Kilifi.