Story by Bakari Ali –
Wakaazi wa kaunti ya Kilifi wametahadharishwa dhidi ya kushawishiwa kifedha na wanasiasa wakati taifa linapokaribia uchaguzi wa mwaka 2022.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Kilifi Mums Kibibi Ali amesema huu ni wakati mwafaka wa jamii kuhamasishwa kuhusu jinsi ya kuwachagua viongozi kwa kuzingatia uadilifu na maendeleo.
Kibibi amewataka viongozi wa kike walio na nia ya kuwania nyadhfa mbalimbali za uongozi nchini kuzikabili changamoto wanazozikumba katika harakati zao za kutafuta nyadhifa hizo
Kwa upande wake Balozi Sophy Kombe amesema wanawake wana uwezo wa kuongoza katika nyadhifa mbalimbali za uongozi iwapo watajitokeze kuwania nyadhfa hizo.