Story by Ali Chete –
Wanawake wanaoishi na mahitaji maalum katika kaunti ya Mombasa wamelalamikia kutengwa katika maswala yanawalenga wanawake katika jamii.
Akizungumza na Wanahabari katika kaunti ya Mombasa wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani mkurugenzi wa Shirika la Akina mama wanaoishi na walemavu la Tunaweza Charity Chahasi amesema viongozi wa kike katika kaunti hiyo imewatenga hali ambayo imewarudisha nyuma kimaendeleo.
Mwanaharakati huyo amesema itakuwa vyema iwapo mashirika mbalimbali ya kijamii na serikali pamoja na viongozi wa kike watawaweza wanawake wanaoishi na mahitaji maalumu basi jamii itanufaika zaidi kimaendeleo.
Kwa upande wake Afisa wa maswala ya nyanjani wa Shirika la mawakili wa kike nchini FIDA Everlyn Otieno amesema jamii imewasahau watu hao na ni muhimu kuwatambua ili wawezekupata haki sawakama watu wengine.