Story by BakarI Ali –
Wanawake nchini wameshauriwa kuungana na kupiginia viti mbalimbali vya kisiasa bila ya kushurutishwa na wanasiasa wa kiume wakati taifa linapokaribia uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.
Naibu Mkurugenzi wa shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la Haki Africa Salma Hemed amesema ni sharti wanawake wawe na misimamo dhabiti ili kuepuka kutumiwa vibaya kisiasa.
Akizungumza katika kaunti ya Kilifi, Salma ameitaka idara ya usalama, wanaharakati na wadau mbalimbali katika kaunti ya Kilifi kushirikiana ipasavyo na kutatua mizozo ya ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Wakati uo huo, amewataka wanawake kuisoma na kuielewa kwa kina katiba ya nchi ili waweze kutambua haki zao za kimsingi.