Wanawake wajawazito katika kaunti ya kilifi wamehimizwa kuanza kliniki mapema ili kupata dawa za kujikinga na ugonjwa wa malaria kabla ya ujauzito kukomaa.
Mshirikishi wa kukimu na kuzuia maambukizi wa ugonjwa wa malaria kaunti hiyo Bi Grace Baya amesema kuwa mwanamke mja mzito anafaa kupata kinga ya malaria kuanzia mwanzo wa ujauzito hadi atakapojifungua.
Bi Grace amesema kuna madhara mengi iwapo mwanamke mja mzito hatopata kinga dhidi ya malaria ikiwemo kuavya ujauzito wake, kuzaa mtoto mwenyezani wa chini au hata kupoteza maisha.
Taarifa na Mariam Gao.