Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Kids Care (KC) Ali Mwaziro amewataka wamama waja wazito kuelekea kliniki mimba zao zinapofikisha miezi mitatu ili kuchunga afya ya mimba zao.
Akizungumza wakati wa kufungua rasmi shule ya watoto walemavu ama wenye uwezo maalum (cerebral palsie) katika shule ya msingi ya Vitsangalaweni huko Lungalunga, mwaziro amewataka wamama wenye watoto walemavu kujitokeza na kuondoa dhana kwamba wamerogwa.
Aidha amesema kuwa kutembelea hospitali mara kwa mara kutawasaidia kulinda vyem mimba zao na kuzaa watoto walio na afya pamoja na maumbile mazuri.
Aidha mwaziro amesema kuwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na serikali ziko tayari kusaidia watoto walemavu.
Vile vile Mwaziro amesema kwamba licha ya changamoto ambazo wamama wenye watoto walemavu wanazipitia amewataka kujitokeza kwani jamii, serikali na mashiriki yasiokuwa yakiserikali wamewakubali kama sehemu nyengine ya jamii.
Naye naibu kamishna wa gatuzi dogo la Lungalunga Josphat Biwoti amesema kwamba serikali inatumia machifu na wahudumu wa kiafya wa kijamii kuzunguka kila wiki ili kuhakikisha kwamba wamama waja wazito wanakwenda kliniki.